Jumatano 10 Juni 2026 - 16:36
Malengo ya siri ya watawala wa Bahrain yaliyo sababisha kupiga marufuku maombolezo ya Muharram nchini humo

Hawza/ Latifa al-Husseini, mwandishi wa habari kutoka Lebanon, amesema: Serikali ya Bahrain katika miezi ya hivi karibuni haijaacha kuwafuatilia na kuwakamata raia wa Kishia kwa visingizio vya kisiasa tu, si vya jinai.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Latifa al-Husseini, mwandishi na mwanahabari wa Lebanon amesema: Serikali ya Bahrain imekwishamtambua adui wake wa moja kwa moja. Katika miezi ya hivi karibuni, haijaacha kuwafuatilia na kuwakamata raia wa Kishia kwa sababu za kisiasa pekee, si za jinai. Sera ya kuyalenga makundi maalumu sasa imekuwa wazi dhidi ya upande mmoja maalumu wa taifa, wakati wa mashambulizi ya Kizayuni-Kimarekani dhidi ya Iran na baada ya hapo, Wizara ya Mambo ya Ndani ilikusanya orodha ya watu wanaotafutwa kwa kosa la kuonesha mshikamano na Iran au kuamini Wilayat al-Faqih.

Aliongeza kuwa: Wapo wanaoamini kuwa njia hii ni ya kuficha janga la kuihusisha nchi katika miradi ya kivita ya Wamarekani katika eneo hili; hata hivyo, matokeo yake yameleta dhulma ya wazi ambayo imeelekezwa kwa upande mmoja maalumu wa taifa; upande ambao mchana na usiku unatuhumiwa kwa uchochezi na usaliti.

Al-Husseini aliendelea kusema: Baada ya mwaka 2011 na kuimarika kwa mkono wa chuma wa vyombo vya usalama ndani ya nchi, serikali ilianza kampeni kubwa za matangazo kwa anuani ya “kuishi pamoja na wengine” na “ustahimilivu” ili kuboresha taswira yake mbele ya maoni ya umma wa Magharibi na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu; lakini utendaji wake katika miaka yote hii umethibitisha kwamba: “Asiye na sifa yenyewe hawezi kumpa mwingine sifa hiyo.” Na yule anayeamini katika fimbo ya usalama hawezi kumkubali mwingine kuwa mshirika wake katika nchi.

Alibainisha kwamba; kutokana na ongezeko la kukamatwa nchini Bahrain katika miezi mitatu iliyopita, ni muhimu kuuliza wataalamu wa sheria kuhusu hali ya kukamatwa huko na hali inayowasubiri Wabahrain.

Baqir Darwish, Mwenyekiti wa “Chama cha Haki za Binadamu cha Bahrain”, ambaye anafuatilia ongezeko la kukamatwa kwa kila siku ndani ya Bahrain, amesema katika mazungumzo na tovuti ya habari ya Al-Ahd: “Tangu kuanza kwa vita dhidi ya Iran, yaani tangu mwezi Februari hadi leo, tumerekodi kesi 474 za kukamatwa kiholela, ambazo miongoni mwao wamo wanawake 7, watoto wasiopungua 27 na zaidi ya wanazuoni wa kidini wa Bahrain 40.”

Kwa mujibu wa Darwish, namna ya kulenga watu na kutengeneza mafaili ya kiusalama inaonyesha kwamba hatua zinazochukuliwa na utawala zinaendeshwa kwa misingi ya chuki, na bila shaka hazitapata mtetezi katika jumuiya ya kimataifa ya sheria.

Anaamini kwamba; anayepaswa kushutumiwa kwa kudhoofisha mamlaka ya kitaifa ni utawala wenyewe, ambao umeivunja mamlaka hiyo kwa kuruhusu sehemu ya mamlaka ya kiusalama kuchukuliwa kupitia Kikosi cha Tano cha Marekani na nafasi yake katika vita vya mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Darwish, akizungumzia mashtaka ya hivi karibuni dhidi ya waliokamatwa, alieleza kwamba; yule anayepinga miradi ya kuhalalisha uhusiano na Israel hapaswi kujaribu kuthibitisha uzalendo wake, bali anayepaswa kuwajibika ni yule anayeitoa mhanga mamlaka ya kitaifa kwa maslahi ya Marekani na Israel kwa ajili ya kuigawa kanda hii.

Akisisitiza kwamba; ubaguzi wa kimadhehebu nchini Bahrain ni miongoni mwa nyenzo za kisiasa za chuki ambazo utawala huzitumia kila unapohitaji kulipiza kisasi zaidi, alieleza kwamba; baadhi ya wafungwa wa kimtazamo wamekuwa wakinyimwa mara nyingi haki ya kutekeleza ibada zao za kidini; mfano wa wazi wa hivi karibuni ni marufuku ya kusimamisha Swala ya Ijumaa ya pamoja katika Msikiti wa Imam Sadiq (a.s) katika eneo la Al-Diraz, kwa sababu khutba za Swala ya Ijumaa zilionesha mshikamano na Palestina pamoja na Lebanon.

Kwa mujibu wa Darwish, nchini Bahrain, ikiwa vyombo vya habari vitapotosha ukweli vitaendelea kuwepo, na utawala hautakuwa na tatizo lolote kuvihusu.

Darwish alieleza kuhusu mpango wa serikali kwamba; utawala unatekeleza mradi mpana zaidi kuliko mashambulizi ya kiusalama yaliyofanyika katika miaka 15 iliyopita. Kwa mujibu wa tathmini za awali na kwa msingi wa yaliyojitokeza katika kauli za Waziri wa Mambo ya Ndani, mzunguko wa mradi huu mpya ni mpana zaidi kuliko Ripoti ya Bandar (Salah al-Bandar, mshauri wa zamani wa Baraza la Kifalme ambaye mwaka 2006 alifichua mifumo ya kuwaondoa Shia).

Aliongeza: “Tunakabiliwa na kampeni ya kung'oa mizizi ya vipengele vyote vya nguvu vya jamii ya Kishia nchini Bahrain; kampeni ambayo inalenga mifumo ya shughuli za Kiislamu ambazo kwa miaka mingi zimeendelea kuwa huru na ambazo sheria za kimataifa zimezihakikishia uhuru huo. Hii inaeleza kwa nini wimbi la kwanza la ukandamizaji liliwalenga wanazuoni wakubwa wa dhehebu hilo, maimamu wa Ijumaa na Jamaa, wakurugenzi wa vyuo vya kidini na wawakilishi wa Marajii wa kidini wa Najaf Ashraf na Qum Tukufu. Wanataka kukomesha mfumo wa jadi wa shughuli za Kiislamu nchini Bahrain na kuigeuza taasisi ya kidini kuwa chini ya udhibiti kamili wa serikali na kuifanya kuwa mfano wa ‘wahubiri wa watawala’. Malengo hayo ni ya muda mrefu, na huenda utawala ukatushangaza kwa hatua zaidi kabla ya Muharram.”

Ashura... lengo linalofuata

Darwish hapa alieleza kwamba; uamuzi wa utawala kuhusu Wakfu wa Jaafari unaashiria nia yake kuhusu siku za Ashura (mwezi wa Muharram). Walianza kwa kuwakamata wahubiri, wasomaji wa mashairi ya maombolezo na waendeshaji wa mawakibu, na hakuna shaka kwamba wanataka kudhibiti maudhui ya hotuba za kidini za Ashura, mashairi ya mawakibu na masharti yote ya uendeshaji wa shughuli hizo ikiwemo ratiba na mambo mengine. Lakini mwenye historia ndefu ya uzoefu nchini Bahrain pia ana uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo.

Darwish katika muktadha huu alikumbusha yale ambayo Wabahrain walikabiliana nayo katika miaka ya themanini, wakati mawakibu zilipolengwa na jambo hilo likageuka kuwa moja ya maeneo ya makabiliano ya kidini na kisiasa dhidi ya utawala.

Mwishoni, Darwish alisema kuhusu hali ya baadaye nchini Bahrain: Mfumo wa mahakama utakuwa mkali katika adhabu na hukumu zinazotolewa kwa msingi wa mashtaka yaliyotengenezwa dhidi ya waliokamatwa.

Alisema kwamba; jambo hili linatokana na hatua za kiusalama na kimahakama ambazo utawala umeendelea kutumia tangu siku ya kwanza, pamoja na taarifa za Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu katika kesi za kimedia kabla ya mahakama, kuingizwa kwa siasa katika mfumo wa mahakama na matumizi ya Ofisi ya Mashtaka ya Makosa ya Kigaidi kama chombo cha kisiasa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha